Kenya kufuta utaratibu wa wanafunzi wa shule za msingi kukaa bweni

0
68

Katibu Mkuu wa Elimu ya Msingi nchini Kenya, Dkt. Belio Kipsang ametangaza mpango wa kuondoa utaratibu wa shule za bweni katika shule za msingi kuanzia darasa la kwanza hadi darasa la tisa kuanzia mwakani 2023.

Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa kongamano la wakuu wa shule za msingi mjini Mombasa, Dkt. Kipsang amesema Serikali ya ‘Kenya Kwanza’ imefanya uamuzi huo kwa lengo la kuwasaidia watoto kukua chini ya uangalizi mzuri wa wazazi wao.

Makamu wa Rais Argentina ahukumiwa jela miaka sita

“Lazima tutengeneze njia ambayo tunaweza kuwa na watoto wetu, na njia pekee ni kupitia shule ya kutwa,” amebainisha Dk. Kipsang.

Inakadiriwa kuwa ikiwa hatua hiyo itatekelezwa, pendekezo hilo litalazimisha angalau asilimia 28 ya wanafunzi katika shule za msingi za bweni kuhamia shule za kutwa.

Send this to a friend