Kenya: Maafisa wa Polisi washikiliwa kwa kumminya mtuhumiwa sehemu za siri

0
58

Maafisa watatu wa polisi nchini Kenya wanashikiliwa kwa tuhuma za kumtesa na kukandamiza viungo vya uzazi vya mwanamume aliyekuwa ameshikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Homa Bay.

Mahakama Kuu ya Migori siku ya Alhamisi imetupilia mbali maombi ya dhamana ya maafisa hao watatu, Peter Langat, Peter Nyakundi na Gilbert Aloka ambao wote wanadaiwa kufanya vitendo hivyo vya ukatili kwa makusudi.

Siku ya tukio, maafisa hao wanadaiwa kumpiga viboko mwanaume huyo aitwaye Edward Ondiek na kisha kumsimamisha katikati ya meza mbili na kutumia koleo kumuumiza sehemu zake za siri, mashtaka ambayo wote wameyakana.

Zanzibar yapiga marufuku wamasai kutembea na silaha

Mwendesha mashtaka wa serikali amelalamika juu ya tishio la kuingiliwa kwa mashahidi na washukiwa kujaribu kuwashawishi baadhi ya wenzao ambao pia ni mashahidi katika kesi.

Send this to a friend