Kenya: Mahakama Kuu yasitisha tozo za miamala kati ya benki na simu

0
42

Mahakama Kuu nchini Kenya imeamuru Safaricom pamoja na benki kuu kusitisha tozo kwa miamala inayofanywa kati ya benki na M-Pesa mpaka pale kesi itakapoamuliwa.

Mahakama ilitoa maagizo hayo Alhamisi Januari 12, 2023 ikisubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa ombi la kupinga kurejeshwa kwa tozo hiyo na kampuni zinazotoa huduma ya pesa kwa njia ya simu.

Ombi hilo liliwasilishwa mwaka jana baada ya amri iliyotolewa na Benki Kuu ya Kenya kutangaza kurejeshwa kwa malipo hayo kuanzia Januari 1, 2023.

Taarifa ya TCRA kuhusu vocha za simu kupandishwa bei

Amri hiyo inajiri baada ya raia wa Kenya, Moses Wafula, kuwasilisha ombi la kupinga kurejeshwa kwa malipo hayo baada ya kusimamishwa kazi mwaka 2020 kutokana na UVIKO19 na kudai kuwa ni ukiukaji wa haki zake na za umma.

Wafula amedai iwapo mahakama itaona kuwa malipo ya M-Pesa ni kinyume cha sheria, fedha zaidi kutoka kwa wananchi zitakuwa zimepotea na huenda ikawa vigumu kuziomba benki zirudishe pesa hizo.

Send this to a friend