Kenya: Mahakama yazuia akaunti 15 za benki za Mchungaji Ezekiel

0
42

Mahakama nchini Kenya imeagiza kuzuiliwa kwa akaunti 15 za benki zinazomilikiwa na Mchungaji Ezekiel Odero kwa siku 30 kutokana na shutuma za utakatishaji fedha.

Hii inafuatia ombi lililowasilishwa na Ofisi ya Mkurungenzi Mkuu wa Upelelezi wa Mashitaka (DCI) kutaka akaunti zote zizuiliwe wakati uchunguzi ukiendelea.

Katika waraka uliowasilishwa mahakamani, DCI, imedai mchungaji huyo wa Kanisa la New Life Prayer Centre anashukiwa kwa utakatishaji wa pesa kutokana na uhusiano na mchungaji Paul Mackenzie wa Kanisa la Good News International ambaye anachunguzwa kwa madai ya kuwalaghai wafuasi wa kanisa lake kufunga hadi kufa ili kukutana na Yesu.

Uganda: Askari 10 wakamatwa kwa kuwaibia wezi

Wapelelezi wameiambia mahakama kuwa akaunti za benki za mchungaji huyo zimekuwa zikipokea kiasi kikubwa sana cha pesa ambazo pesa zake zinashukiwa kuwa haramu zilizotoka kwa wahanga ambao wanadaiwa kulaghaiwa kuuza mali zao na kumpatia mchungani Mackenzie.

Siku chache zilizopita mchungaji huyo aliitaka mahakama kuu ya mjini Mombasa kuzuia kufujwa kwa akauntu zake akidai kuwa kushikiliwa kwa akaunti zake kutakuwa ni kuingilia uhuru wake na kanisa lake kwa ujumla.

Send this to a friend