Kenya: Makaburi yagundulika kanisani, mapya yaibuka

0
56

Timu ya usalama kutoka taasisi mbalimbali nchini Kenya imegundua makaburi manne katika kanisa moja jijini Kisumu ambapo kulikuwa na watu wanaosadikiwa kuwa na matatizo ya akili wanaodaiwa kushikiliwa kwa nguvu bila idhini yao.

Timu hiyo ya usalama iliyojumuisha maafisa kutoka Idara ya Upelelezi (DCI), Maafisa wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP), na Maafisa wa Afya ya Umma wa Kaunti ya Kisumu, ilifanya uvamizi katika Kanisa la Holy Ghost Coptic la mhubiri maarufu, John Pesa huko Kisumu baada ya kupokea taarifa kuwa baadhi ya watu waliokuwa katika kanisa hilo huenda walikufa na kuzikwa kwenye eneo hilo bila kujulikana.

Mahakama ya Kisumu iliidhinisha operesheni hiyo ambayo ilipelekea kuokolewa kwa watu watatu wagonjwa waliokutwa eneo hilo ambao walikuwa wameshikiliwa kinyume cha sheria na walionekana kuwa katika hali mbaya ya afya ya akili.

Niger yakata uhusiano wa kidiplomasia na Nigeria, Ufaransa, Marekani na Togo

“Hii inafuata amri ya mahakama ambayo iliidhinisha taasisi ya uchunguzi kufanya operesheni hiyo baada ya malalamiko kadhaa kuwa watu wenye changamoto za akili walikuwa wameshikiliwa kinyume cha sheria ndani ya eneo la kanisa na kuwa kunaweza kuwa na shaka kuwa baadhi yao walikufa na kuzikwa kwenye eneo la kanisa kinyume cha taratibu,” imesema taarifa ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP).

Imeongeza “Katika operesheni hiyo, maeneo mawili yaliyofanana na makaburi yaligunduliwa nyuma ya kanisa na watu watatu waliotuhumiwa kuwa wagonjwa waliokutwa waliokolewa na kupelekwa hospitalini kwa uchunguzi na matibabu.”

Send this to a friend