Mama na binti yake wakamatwa wakicheza kwenye kaburi la mchungaji

0
43

Mama na binti yake mdogo anayesoma darasa la sita, wamenusurika kuuliwa na watu wenye hasira kali baada ya kudaiwa kunaswa wakicheza kwenye kaburi la mchungaji katika kijiji cha Roura, Mugirango Kusini kaunti ya Kisii nchini Kenya.

Vyanzo vya habari vimesema kuwa washukiwa hao wawili walikamatwa na kundi la vijana waliokuwa wakikesha katika nyumba hiyo Jumamosi iliyopita saa tano usiku.

Mwili wa Mchungaji wahifadhiwa mwaka mzima wakingojea afufuke

kulingana na wakazi wa eneo hilo, Kaburi hilo jipya lilikuwa na mabaki ya mchungaji wa kiinjilisti, Rev Alloys Mogoi ambaye alizikwa Ijumaa iliyopita.

Kisa hicho kimethibitishwa na Chifu, Charles Omwono ambaye amebainisha kuwa afisa aliyekuwa likizo alimsaidia kudhibiti hali hiyo na kuwaokoa washukiwa hao dhidi ya kushambuliwa.

“Niliamshwa na sauti za vijana wenye hasira waliokuwa wanataka kuwashambulia washukiwa. Mwanamke huyo na binti yake walipelekwa katika kituo cha Polisi cha Etago kusubiri kufikishwa mahakamani,” amesema Chifu Omwono.

Send this to a friend