Kenya: Mawaziri kubinafsisha Mashirika ya Umma bila idhini ya Bunge

0
23

Baraza la Mawaziri limeidhinisha Muswada wa Ubinafsishaji wa mwaka 2023 ambao utabatilisha sheria ya ubinafsishaji ya mwaka 2005 unaotoa mamlaka kwa hazina (Serikali) kubinafsisha mashirika ya umma bila idhini ya bunge.

Uidhinishaji huo unamaanisha kuwa muswada unaofadhiliwa na serikali utawasilishwa hivi karibuni na kiongozi wa wengi katika Bunge la Kitaifa, Kimani Ichungw’ah huku serikali ikilenga kufupisha mchakato wa kuuza mashirika hayo ya umma.

Baadhi ya mashirika ambayo serikali inakusudia kubinafsisha ni pamoja na Chemelil Sugar, South Nyanza Sugar, Kabarnet Hotel, Mt Elgon Lodge, Golf Hotel na Nzoia Sugar, Miwani Sugar, Sunset Hotel Kisumu, Kenya Safari Lodges and Hotels, Consolidated Bank, Development Bank of Kenya, Agro-Chemical and Food Company, Kenya Wine Agencies, Kenya Meat Commission na vyuo vikuu vya umma.

TCRA yavionya vyombo vya habari kuhusu taarifa za kidini za kufikirika

“Hii inaleta mfumo wa kisheria na sera wezeshi zaidi ambao utasimamia ubinafsishaji nchini,” limesema Baraza la Mawaziri likiongeza kuwa uuzaji wa mashirika ya umma yasiyo ya kimkakati na yasiyofanya kazi utasaidia kufadhili uboreshaji wa miundombinu na kuboresha utoaji wa huduma kwa Wakenya.

Muswada huo pia unalenga kugeuza Tume ya Ubinafsishaji kuwa shirika la serikali litakaloitwa Mamlaka ya Ubinafsishaji, ambalo litakuwa na makao yake hazina.

Ubinafsishaji wa mashirika ya umma umeibuka kama kipaumbele katika mpango wa ujumuishaji wa kifedha wa Rais William Ruto, na mapato kutoka kwa mauzo yanawekwa katika hazina ya pamoja kwa ajili ya matumizi ya bajeti.

Send this to a friend