Kenya: Msichana wa miaka 15 awaua ndugu zake wanne

0
42

Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) nchini Kenya, wanachunguza tukio la msichana wa miaka 15 anayedaiwa kuwaua wadogo zake watatu na binamu yake .

Kulingana na DCI, mwanafunzi huyo wa kidato cha kwanza kutoka Kaunti ya Kiambu amekiri kutekeleza uhalifu huo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Akiwa katika kituo cha Polisi cha Kikuyu, mshukiwa huyo alikiri kwa wapelelezi kufanya mauaji hayo na jinsi alivyowaua wadogo zake wenye umri wa miezi 15, miaka 5, na miaka 7 kati ya Februari na Julai 2021.

Mshukiwa pia alikiri kwamba mwezi uliopita alimuua binamu yake, ambaye alikuwa na umri wa miezi 20 kwa kumzamisha kwenye kisima cha nyumba yao katika kijiji cha Gathiga, kaunti ndogo ya Kabete.

“Mtoto huyo alikiri kutekeleza mauaji hayo mbele ya afisa wa watoto katika kaunti ndogo ya Kikuyu. Kwa sasa yuko kizuizini katika kituo cha polisi cha Kikuyu huku wapelelezi wakimshughulikia ili afikishwe mahakamani,” DCI iliripoti.

Send this to a friend