Kenya: Mtanzania ahukumiwa miaka 30 jela kwa usafirishaji haramu wa watoto

0
40

Raia wa Tanzania aliyekamatwa nchini Kenya kwa kusafirisha watoto wadogo kutoka sehemu mbalimbali nchini, James Sengo Nestroy amehukumiwa kifungo miaka 30 jela.

Mwanaume huyo alikamatwa baada ya kubainika anajihusisha na usafirishaji haramu wa watoto na watu wenye ulemavu ambapo aliamriwa na mahakama, alipe faini ya TZS milioni 564 au atumikie kifungo jela.

Sengo ambaye ameishi nchini Kenya tangu 2001, alikamatwa mwaka jana kufuatia kufichuliwa na idhaa ya Afrika ya Shirika la la Utangazaji Uingereza (BBC Africa) kuhusu wizi na uuzaji wa watoto wachanga nchini Kenya.

Baadhi ya waathirika wa biashara hiyo wengi wakiwa ni wenye ulemavu na raia wa Tanzania walidai mwanaume huyo aliwaahidi kazi nzuri wakifika Kenya lakini waliishia kutumikishwa katika kazi za kuombaomba.

Mwanaume apigwa kwa kuiba nguo za ndani za wanawake

“Ushahidi unathibitisha kuwa mshitakiwa alikuwa akimtumia vibaya mwathiriwa kwa ajili ya kujinufaisha kiuchumi kwa kutumia vibaya udhaifu wake na hadhi yake kama mtu anayeishi bila kuhama baada ya kumsafirisha kutoka Tanzania,” amesema Hakimu Agnes Mwangi.

Send this to a friend