Kenya: Mwanafunzi achomwa kisu kisa msichana, wanakijiji wachoma nyumba za washukiwa

0
54

Mwanafunzi wa kidato cha nne ameuawa huku nyumba tisa zikiteketezwa na mifugo kuibwa katika Kijiji cha Musunji, Cheptulu, Kaunti ya Vihiga, kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mgogoro wa mapenzi.

Kulingana na ripoti, kijana huyo aliyetambulika kwa jina la Clinton aliuawa kwa kuchomwa kisu na wenzake siku moja tu kabla ya kuanza kwa mitihani ya Kenya Certificate of Secondary Education (KCSE) kufuatia mzozo kuhusu msichana anayeishi katika kijiji hicho.

Kujibu tukio hilo la kijana huyo, wakazi wa kijiji hicho wamezishambulia nyumba za washukiwa kwa moto, na kisha kukatakata mazao kutoka kwenye mashamba watuhumiwa.

Mtoto wa miaka 14 ashikiliwa kwa tuhuma za kubaka na kulawiti

Kulingana na Kamanda wa Polisi wa eneo hilo, Hamisi Ruth Langat amebainisha kuwa washukiwa wawili tayari wamekamatwa kufuatia shambulio hilo.

Send this to a friend