KENYA: Rais Ruto afufua mpango wa ushirikiano na sekta binafsi kuendesha bandari tano

0
43

Serikali ya Kenya chini ya Rais William Ruto imepanga kuingia ushirikiano na sekta binafsi (PPP) kuendesha na kusimamia bandari tano muhimu mapngo wenye thamani ya Ksh 1.4 trilioni [TZS trilioni 23.9] ili kufufua sekta ya baharini nchini humo.

Shirika la Maendeleo la Kenya (KDC), taasisi ya fedha ya maendeleo, imefichua kuwa utawala wa Kenya Kwanza unatafuta waendeshaji wa sehemu za bandari ya Kilindini, Bandari ya Dongo Kundu, Bandari ya Lamu, Bandari ya Kisumu na Bandari ya Uvuvi ya Shimoni katika kile kinacholengwa kuwa ni kuifanya ukanda wa kaskazini kuwa wa ushindani.

“Bandari zinakabiliwa na changamoto ya msongamano na hivyo, mizigo kukaa kwa muda mrefu. Bandari hizo zitakodishwa au kutolewa kwa waendeshaji binafsi wenye mfumo wa usimamizi wa bandari,” imesema KDC katika mazungumzo yake kwa wawekezaji watarajiwa.

Balozi aliyewafananisha Waafrika na nyani arudishwa kwao

Njia ya biashara ya Kenya hivi karibuni imekuwa katika ushindani mkubwa huku nchi zisizo na bandari kama Uganda, Burundi na Rwanda zikipendelea kutumia njia ya Tanzania katika usafirishaji.

Kwa mara ya kwanza mizigo inayohudumiwa katika Bandari ya Mombasa imepungua ndani ya miaka mitano kutoka tani milioni 34.76 mwaka 2021 hadi tani milioni 33.74 mwaka 2022, sababu kubwa ikitajwa ni ushindani kutoka Bandari ya Dar es Salaam.

Aidha, Serikali ya Kenya inatafuta uwekezaji wa TZS bilioni 719 kutoka sekta binafsi kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika bandari ya Lamu.

Send this to a friend