Kenya: Serikali yapandisha bei ya umeme kwa hadi asilimia 63

0
9

Bei ya umeme nchini Kenya inatarajiwa kuongezeka kwa hadi asilimia 63 baada ya mdhibiti wa sekta ya nishati kuidhinisha ushuru wenye gharama kubwa wa Kenya Power ambayo inalenga kukusanya pesa zaidi ili kufadhili uboreshaji wa mifumo yake ya zamani ya usambazaji.

Katika ukaguzi wa kwanza wa ushuru wa umeme tangu 2018, Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) imepandisha bei hadi KSh12.22 [TZS 217.8] kwa uniti kutoka KSh10 [TZS 178.2] kwa wale wanaotumia chini ya uniti 30 sawa na ongezeko la asilimia 22.2.

Kenya: Uhaba wa mahindi, Serikali yashauri wananchi kula wali

Pia imeongeza gharama zaidi kwa watumiaji wanaotumia kati ya uniti 30-100 kutoka KSh10 [TZS 178.2] hadi KSh16.3 [TZS 290.5], ongezeko la asilimia 63, kuanzia Aprili mwaka huu.

Aidha, kwa wale wanaotumia zaidi ya uniti 100 za umeme sasa watalipa KSh 20.97 [TZS 373.8] kwa uniti kutoka KSh 15.8 [TZS 281.6] ikiwa ni ongezeko la asilimia 32.

“Watumiaji hawa watapewa ruzuku kutoka kwa vikundi vingine vya watumiaji ili kuwalinda wanajamii waliohatarini. Licha ya punguzo hili, kitengo cha Ushuru wa Lifeline kitachangia wateja milioni 6.3, sawa na asilimia 71.31 ya idadi ya watumiaji wote.” imesema EPRA.

Send this to a friend