Kenya: Uchumi mbaya wapelekea baa kubuni mbinu mpya ili vinywaji vinunuliwe

0
39

Kutokana na hali ngumu ya kiuchumi nchini Kenya, wamiliki wa baadhi ya baa wamebuni mbinu mpya za kugawa karanga za bure, njugu na nyama choma kwenye baa zao ili kuwashawishi wateja kununua vinywaji zaidi.

Mmoja wa wamiliki wa baa nchini humo, Jeremy Kamau ameiambia The Citizen kwamba tangu kuzuka kwa janga la UVIKO-19 mwezi Aprili, 2020 uchumi umekuwa si mzuri hivyo kufanya idadi ya wateja kupungua.

“Watu wengi wamegundua kwamba wanaweza kununua vinywaji kwa bei nafuu kutoka kwenye maduka ya pombe na maduka makubwa na kunywa nyumbani,” amesema Kamau.

Mmoja wa wateja kweye baa hizo, Junior Mitch amesema wakati wanapotafuna njugu na karanga, kila mara huhisi kiu na kununua vinywaji zaidi hali ambayo inawapa faida wamiliki wa baa.

Send this to a friend