KENYA: Uchunguzi wabaini Mackenzie aliwaua waumini waliobadili mawazo au waliochelewa kufariki

0
16

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Kenya, Prof. Kithure Kindiki amesema mhubiri mwenye utata, Paul Mackenzie wa kanisa la Good News International Church aliajiri watu wenye silaha kuwachunga wafuasi wake kufunga mpaka pale watakapokufa kwa njaa.

Akizungumza mbele ya kamati ya Seneti inayochunguza tukio hilo siku ya Ijumaa, amesema Mackenzie alitumia genge lililomiliki silaha za jadi kuwaua baadhi ya waumini waliochukua muda mrefu kufa na wale waliobadilisha mawazo yao wakati wa kufunga.

“Mackenzie alikuwa ameajiri vijana wenye silaha ili kuzunguka wafuasi wake na kusimamia njaa yao hadi kufa. Wafuasi waliobadili mawazo yao kuhusu njaa waliuawa kwa kunyongwa au kupigwa na vitu butu,” amesema.

Ufafanuzi wa Polisi kuhusu madai ya Kigwangalla kumpiga risasi mlinzi

Hata hivyo amesema katika uchunguzi uliofanywa umebaini watu hao walilishwa vizuri, milo mitatu kwa siku, tofauti na ambavyo aliwaagiza waumini wa kanisa lake.

Maafisa wa polisi wanaamini kwamba miili mingi ni ya waumini wa kanisa la Mackenzie anayedaiwa kuwaagaiza kufunga hadi kufa ili kukutana na Yesu huku Mwanapatholojia Mkuu, Johannsen Oduor akibainisha kuwa baadhi ya waathiriwa wakiwemo watoto walinyongwa, kupigwa hadi kufa na kufunikwa pua na mdomo.

Send this to a friend