Kenya: Waandamanaji wavamia shamba la Rais Kenyatta

0
23

Mamia ya waandamanaji waliokuwa na silaa wamevamia shamba linalomilikiwa na familia ya aliyekuwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta siku ya Jumatatu asubuhi katika maandamano yanayoendelea nchini humo.

Watu hao wasiojulikana walivamia ardhi ya Kenyatta iliyoko kando mwa barabara ya Nairobi Eastern Bypass, na kukata miti pamoja na kuwaondoa kondoo saa chache baada ya kiwanda cha gesi cha kiongozi wa muungano wa Azimio La Umoja One Kenya, Raila Odinga kushambuliwa na madirisha kuvunjwa.

Nigeria yakumbwa na uhaba wa fedha

Hata hivyo, Odinga amemlaumu Naibu Rais, Rigathi Gachagua kufuatia uvamizi huo wa ardhi na kiwanda chake cha gesi cha East Africa Specter Limited akidai kuwa kiongozi huyo aliwatuma waporaji hao kufanya uharibifu huo pamoja na Rais Kenyatta.

“Waoga hao walituma majambazi leo kwenye shamba la Uhuru Kenyatta. Pia wameamua kupeleka watu kwenye kiwanda changu cha Specter. Hicho ni kitendo cha uhalifu na kijinga,” Odinga aliwaambia waandamanaji katika eneo la Kibera Nairobi.

Biashara nyingi katikati mwa jiji zimefungwa kutokana na maandamano nchini humo huku mtu mmoja akiripotiwa kuuawa wakati wa shambulio la polisi na waandamanaji walipojaribu kuwarushia mawe, kuchoma matairi na kuziba barabara kuu.

Send this to a friend