Kenya: Wananchi waacha magari majumbani kutokana na bei kubwa ya mafuta

0
27

Wakati Tanzania bei ya mafuta ikishuka, nchini Kenya matumizi ya mafuta yamepungua kwa mara ya kwanza tangu 2017, ikiashiria hali ya uchumi kudorora huku kukiwa na bei ya juu ya mafuta na kupungua kwa mauzo ya magari.

Matumizi ya petroli ambayo hutumiwa sana na wamiliki wa magari ya binafsi, yamepungua kwa kasi hadi tani milioni 1.508 kutoka tani milioni 1.544 mwaka uliopita, ikiashiria kupungua kwa matumizi ya magari binafsi.

Polisi: Madereva watembee na vyeti vya udereva, tutavikagua

Matumizi ya mafuta yalipungua kwa mwaka mmoja huku gharama ya rejareja kwa lita moja ya dizeli ikipanda kwa asilimia 32.18 hadi Sh144.38 [TZS 2,539.2] kwa wastani jijini Nairobi huku ile ya petroli ikipanda kwa asilimia 23.90 hadi Sh154.77 [TZS 2,722].

Gharama ya juu ya bidhaa hiyo muhimu, kichocheo kikuu cha shughuli katika sekta muhimu kama vile kilimo na uchukuzi, ilisababisha uongozi uliopita kutumia Sh81 bilioni [TZS trilioni 1.4] kama ruzuku katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 2022 ili kuwanufaisha watumiaji.

Utawala wa Rais William Ruto, uliondoa ruzuku hiyo kuanzia Septemba mwaka jana mara tu baada ya kuchukua mamlaka, kwa maeezo kuwa ruzuku hiyo ilikuwa ikiigharimu Serikali kiwango kikubwa cha fedha.

Kupungua kwa matumizi ya mafuta kunadhihirisha kupungua kwa shughuli za kiuchumi mwaka jana, kulikochangiwa pia na ukame, kupanda kwa mfumuko wa bei, na riba kubwa za mikopo ambavyo kwa pamoja vimeathiri biashara na uwekezaji.

Send this to a friend