Kenya: Wanawake wanawalipa wanaume milioni 5 wawape mimba

0
11

Biashara ya kununua mbegu za wanaume imeshamiri katika Kaunti ya Murang’a nchini Kenya ambapo baadhi ya wanawake wanajitolea kulipa hadi Ksh 300,000 [TZS milioni 5.1] ili kupata mimba.

Wanaume ambao wanapendelewa zaidi katika biashara hii ni wale wenye umri kati ya miaka 20 hadi 40 na wanahitaji kuwa na sifa ambazo wanawake hao wanavutiwa nazo ikiwemo watu wenye akili na wengine hupendelea wanaume ambao ni warefu na wenye rangi ya ngozi ya wastani, yaani sio weupe sana wala weusi kupindukia.

Mmoja wa wanawake hao ameiambia gazeti la Taifa Leo kuwa wanawake wa siku hizi ambao wameamua kujitegemea kimaisha hawataki kuingia katika ndoa na badala yake wanatafuta tu mbegu ili waweze kuzaa na kulewa watoto wao.

“Hata hivyo, tunazingatia sana suala la kuwa na watoto wenye sura nzuri na pia akili nzuri ili waweze kufanya vizuri katika masomo,” amesema mwanamke huyo.

Mahakama yaamuru nyumba iuzwe kulipia deni la mahari

“Mwanamume huyo lazima akubali kupimwa magonjwa hatari ya kizazi na magonjwa ya zinaa. Akipita vipimo hivyo, anatakiwa kutumia dawa za kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi wakati wa ngono na akubali kuishi nami ili asitafute mwenzi mwingine na kunipatia maambukizi,” amesema mwanamke mwingine ambaye tayari analea mapacha wa miezi mitatu aliowapata kupitia mradi huo.

Aidha, imeelezwa kwamba wanaume wanaouza mbengu zao hutakiwa kusaini mkataba unaosema kuwa jukumu lake ni kutoa mbegu za uzazi tu na sio malezi, na baada ya kukamilika kwa mkataba huo, ataacha uhusiano wake na mtoto pamoja na mama wa mtoto.

Send this to a friend