Kenya: Watumia magunia kama mbadala wa majeneza kuzika

0
16

Baadhi ya wakazi wa Ndindiruku kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya, wamelazimika kuwazika wapendwa wao kwa magunia kutokana na kushindwa kumudu gharama kubwa za mazishi.

“Tunanunua gunia kwa Ksh 50 [takribani TZS 1,000] pekee na kumzika mtu huyo, na inatuchukua dakika 20 pekee,” amesema mmoja wa wakazi hao.

Ajikuta ndani ya jeneza amezikwa futi sita baada ya kulewa kupita kiasi

Katika kisa kilichotokea hivi karibuni, wakazi wa kijiji hicho waliamua kwenda kumzika mpendwa wao kwa gunia kabla ya kiongozi wa eneo hilo kuingilia kati na kununua jeneza.

“Kwetu Ndindiruku ni kawaida, kwa wale ambao hawajajiunga na vikundi vya mazishi. Juzi ilinichukua dakika 10 kumzika mzee mmoja baada ya familia yake kushindwa kumudu gharama za maziko,” amezungumza mkazi wa eneo hilo.