Kenya yabaini uwepo wa Mbu asiyekufa kwa dawa za Afrika

0
42

Watafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Tiba Kenya (KEMRI) wamegundua mbu aina ya ‘Anopheles Stephensi’ kutoka barani Asia ambaye anastahimili viua wadudu vinavyotumika barani Afrika.

Inadaiwa mbu huyo anaweza kuishi katika msimu wa kiangazi na msimu wa mvua na hata kuweza kuzaliana popote, huku takwimu kutoka hospitalini hapo zikionesha ongezeko la visa vya malaria japokuwa haukuwa msimu wa kawaida wa ugonjwa huo.

Wataalamu wameingiwa na wasiwasi kuwa maambukizi ya malaria sasa yanaweza kuendelea kwa mwaka mzima badala ya kuwa ya msimu.

TMA: Kimbunga ‘Freddy’ hakina madhara ya moja kwa moja

“Kwa bahati mbaya, ugunduzi huu nchini Kenya unaweza kutafsiri kwa kiwango cha juu cha maambukizi ya malaria katika maeneo ya mijini na pembezoni mwa miji nchini, na inaweza kubadilisha mafanikio yaliyopatikana katika vita dhidi ya malaria,” amesema Mkurugenzi Mkuu wa KEMRI, Dkt. Samuel Kariuki.

Aidha, watafiti wamewataka Wakenya kutumia zana zilizopo za kudhibiti malaria kama vile kulala ndani ya vyandarua vilivyotiwa dawa, kutumia dawa za kufukuza mbu na kuvaa nguo za mikono mirefu ili kuzuia kuumwa na mbu.

Barani Afrika, mbu huyo aligunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Djibouti miaka 10 iliyopita na sasa ameonekana Ethiopia, Sudan, Somalia na Nigeria.

Send this to a friend