Kenya yafunga mipaka yake na Tanzania na Somalia kwa siku 30

0
62

Serikali ya Kenya imetangaza kufunga mipaka yake na Tanzania na Somalia kuanzia leo Mei 16, 2020 saa sita usiku ikiwa ni sehemu ya mkakati wa nchi hiyo kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

Uamuzi huo umetangazwa na Rais Uhuru Kenyatta ambapo ameianisha kuwa zuio hilo litahusisha watu pekee, lakini magari ya mizigo yataendelea kuingia nchini humo.

Hata hivyo amesema kwamba madereva wa malori ya mizigo watalazimika kupimwa kwanza kama wana maambukizi ya homa ya mapafu (Covid-19) kabla ya kuruhusiwa kuingia nchini humo.

Mbali na uamuzi huo, nchi hiyo imeongeza muda wa amri ya watu kubaki ndani kwa siku 21 zaidi.

Hadi sasa nchi hiyo imeripoti kuwa na visa 830 vya waathirika wa Covid-19, na kati ya hivyo watu 50 wamefariki dunia huku waliopona wakiwa ni 50.

Send this to a friend