Kenya yakodi ardhi ya kulima mahindi nchini Zambia

0
14

Waziri wa Kilimo nchini Kenya, Mithika Linturi na mwenzake wa Zambia, Mtolo Phiri wametia saini makubaliano ili kupata kati ya hekta 20,000 na 40,000 za ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo kikubwa cha mahindi ili kuilisha nchi ya Kenya.

Lengo ni kutenga ardhi hiyo kwa ajili ya wakulima wa Kenya watakaolima mazao hayo ambayo yatauzwa Kenya baada ya kuvunwa.

Katibu Mkuu wa Kilimo, Kello Harsama amesema matatizo ya mabadiliko ya hali ya hewa yalilazimisha serikali kuzingatia mpango huo.

“Kwa kweli tumeathiriwa sana na ukame na inabidi tufikirie nje ya boksi,” amesema Harsama

Wakati wa kutia saini makubaliano mjini Lusaka, Waziri wa Kilimo Mithika Linturi amesema hatua hiyo itasaidia katika kufikia usalama wa chakula kwa kuwaruhusu wakulima wa Kenya kupata vibali vya kulima mahindi nchini Zambia ili kulisha Wakenya.

Send this to a friend