Kenya yakumbwa na uhaba wa kondomu

0
57

Mashirika ya kiraia nchini Kenya yamelalamikia kuwepo kwa uhaba mkubwa wa kondomu za bure kote nchini humo kutokana na ushuru kuwa mkubwa.

Bidhaa za kuokoa maisha kwa kawaida huagizwa na kusambazwa bila malipo lakini kutokana na ushuru kuwa juu, wasambazaji hawafanyi tena usambazaji wa bidhaa hizo nchini Kenya.

Wanaharakati hao wameitaka Serikali kuondoa ushuru katika bidhaa hizo kwani itasaidia katika kupunguza maambukizi mapya dhidi ya Virusi vya Ukimwi nchini humo.

Kenya inahitaji takribani kondomu milioni 455 kila mwaka, lakini Serikali ina uwezo wa kununua milioni 150 pekee ya bidhaa hizo.

Kenya inarekodi ya maambukizi mapya ya VVU takribani 34,000 kila mwaka. Walakini, tangu 2020 imeripotiwa kuwepo kwa ongezeko la wafanyabiashara wa ngono nchini humo.

Send this to a friend