Kenya yamzuia Rostam Aziz kujenga kiwanda cha gesi

0
42

Kenya imesitisha mpango wa mfanyabiashara, Rostam Aziz kujenga kiwanda na ghala la kuhifadhi gesi katika bandari ya Mombasa hivyo kuhatarisha uhusiano wa kibiashara kati ya mataifa hayo ya Afrika Mashariki.

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli imekataa kupitisha maombi ya Taifa Gas ya kujenga kituo katika eneo maalum la kibiashara huko Dongo Kundu, karibu na Bandari ya Mombasa ikitaja hatari za mazingira zinazotokana na kituo hicho cha gesi cha tani 30,000.

Aidha, matarajio ya Aziz ya kuanzisha biashara ya gesi ya kupikia kwa rejareja nchini Kenya yameonekana kuzua mzozo mwingine wa soko na wafanyabiashara wa mafuta kama vile Vivo, Rubis na Total ambao wateja wao ni asilimia 23.9 ya kaya za Kenya zinazotumia gesi ya petroli iliyoyeyushwa kwa ajili ya kupikia.

Kuingia kwa Taifa gesi nchini Kenya ni sehemu ya mkataba wa kibiashara kati ya Tanzania na Kenya, zilizotiwa saini kati ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Rais Samia Suluhu mwaka jana.

Taifa Gas ambayo zamani ilikuwa Mihan Gas, inafanya kazi kama kampuni kubwa zaidi ya usambazaji wa LPG (Liquefied petroleum gas) Tanzania.

Send this to a friend