Kenya yapokea uwekezaji wa zaidi ya TZS bilioni 600 kutoka Dubai

0
42

Kenya imepokea uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) kutoka Dubai wenye thamani ya dola milioni 253 [TZS bilioni 631.9] kwa kipindi cha miaka mitano, hadi Juni 2023, kulingana na takwimu za fDi Intelligence zinazotolewa na Financial Times. Hii inaonyesha kuongezeka kwa mikataba katika sekta muhimu kama vile usindikaji wa chakula, huduma za kifedha na teknolojia ya habari na programu.

Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dubai Chambers, Mohammad Ali Rashed Lootah amesema wanatarajia FDI kuongezeka zaidi, huku kampuni zaidi kutoka nchi za Ghuba zikiangazia fursa za biashara nchini Kenya na kubainisha kuwa zaidi ya kampuni kutoka Dubai zinatafuta mikataba nchini Kenya.

“Tunaamini daima kwamba biashara na uwekezaji huleta thamani chanya, na kampuni zaidi huko Dubai zinatafuta mikataba nchini Kenya,” amesema wakati akizungumza na Business Daily huko Nairobi kando ya mkutano wa biashara kati ya kampuni za Dubai na Kenya.

Lootah amesema Dubai Chambers imefanya mikutano na mashirika kama KenTrade (Shirika la Mtandao wa Biashara la Kenya) na vikundi vingine vya biashara nchini humo, huku akibainisha kuwa wameleta kampuni 19 kutoka Dubai kwa mikutano ya biashara na wanaamini watapata fursa kubwa kutokana na umuhimu wa soko la Kenya na fursa nyingi za uwekezaji zilizopo.

Ameongeza kuwa thamani ya biashara baina ya Kenya na Dubai isiyohusisha mafuta iliongezeka kwa asilimia saba hadi dola bilioni 2.1 [TZS trilioni 5.2] mwaka uliopita, ikilinganishwa na mwaka uliotangulia.

Send this to a friend