Kenya yasema haijazuia ndege za Tanzania

0
48

Saa chache baada ya Tanzania kuzuia ndege za Shirika la Ndege la Kenya kuingia nchini, serikali ya Kenya imesema kuwa haijazuia ndege za Tanzania kuingia nchini humo.

Akizungumza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi, Waziri wa Uchukuzi nchini humo James Macharia amesema kilochofanyika ni kuwekwa taratibu za kudhibiti virusi vya corona kwa wageni watakaofika Kenya.

“Hatujapiga marufuku nchi yoyote kuingia Kenya. Hatujafunga anga letu, kile tulichofanya ni kuweka utaratibu wa karantini kwa baadhi ya nchi kulingana na tathmini ya janga hilo,” amesema Macharia.

Waziri huyo amesema tayari wamefanya mazungumzo na Tanzania na wamemaliza sintofahamu iliyokuwepo na kabla ya siku kumalizika wananchi wa pande hizo mbili wataruhusiwa kutoka na kuingia katika nchi hizo.

Send this to a friend