Kenya yatangaza siku tatu za maombolezo kufuatia kifo cha Rais Mkapa

0
39

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametangaza siku tatu za maombolezo nchini humo kufuatia kifo cha Mwendazake Rais Mstaafu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa.

Rais Kenyatta ametangaza kuwa maombolezo ya kitaifa yataanza Jumatatu mpaka Jumatano, siku ambayo Mzee Mkapa atazikwa.

Katika kipindi chote cha maombolezo bendera ya Kenya na ile ya Jumuiya ya Afrika Mashariki zitapepea nusu mlingoti.

Rais Mkapa alikuwa na mchango mkubwa katika siasa za Kenya hasa katika masuala ya kidiplomasia.

Ilikuwa ni Mzee Mkapa na Kofi Anan waliokuwa mstari wa mbele katika usuluhishi uliolenga kupatikana kwa amani katika mapigano yaliyofuatia uchaguzi wa mwaka 20017.

Send this to a friend