Kenya yauza mirungi ya TZS bilioni 4 Somalia ndani ya siku nne

0
108

Kenya imeuza mirungi yenye thamani ya TZS bilioni 4.3 nchini Somalia ndani ya siku nne tangu kurejeshwa kwa soko hilo.

Mpaka sasa nchi hiyo imeuza tani 81.4 za bidhaa hizo kwenda Mogadishu huku wafanyibiashara 19 kati ya 22 waliotuma maombi ya vibali vya kuuza bidhaa nje wakiidhinishwa, na wengine zaidi wakitafuta kibali cha kupata leseni.

Zimbabwe yaruhusu bangi kuuzwa kwenye maduka ya dawa

Mwenyekiti wa Nyambene Miraa Trade Association (Nyamita), Kimathi Munjuri amesema kuna mazao ya kutosha katika mashamba ili kukidhi soko nchini Somalia.

Kilo moja ya mirungi hadi Somalia kwa sasa inauzwa kwa TZS 53,622 ambayo bado ni ya chini ikilinganishwa na TZS 58,290 iliyokuwa ikiuzwa kabla soko halijasimamishwa.

Wafanyabiashara wamekuwa wakitegemea soko la ndani katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita baada ya kupigwa kwa marufuku usafirishaji wa zao hilo kufuatia mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, hatua iliyopelekea Kenya kuanza kutafuta soko jipya nchini Djibouti ili kuokoa wakulima wanaotegemea zao hilo kama tegemeo lao kuu kiuchumi.

Send this to a friend