Kenya imeweka zuio la muda usiojulika la uingizaji maziwa ya unga kutoka nje ya nchi ili kuwalinda wafanyabiashara wa ndani na wakulima kutokana na uzalishaji wa ziada na kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo.
Msimu wa mvua unaotarajiwa kuanza nchini humo unaaminika utawezesha uzalishaji wa chakula cha mifugo na kuongeza uzalishaji wa maziwa, hivyo kupunguza uagizaji kutoka nje.
Bodi ya Maziwa Kenya imesema kuwa itaendelea kufuatilia uzalishaji na uhitaji wa maziwa kabla ya kuondoa zuio hilo.
Anayejiita ‘Yesu’ akimbillia polisi, wananchi wataka kumsulubisha Pasaka
Mbali na kuweka zui hilo, bodi pia imeweka zuio katika utoaji wa vibali vya kuingiza maziwa.
Zuio hilo linaaminika kuwa linakwenda kinyume na makubaliano ya biashara huria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya usafirishaji huru wa bidhaa na soko la pamoja.
Uganda na Rwanda ni nchi zinazoongoza kwa kuingiza maziwa Kenya, hivyo zitaathirika zaidi kwa zuio hilo.