Kenya: ‘Yesu wa Tongaren’ awekwa kizuizini kupisha uchunguzi

0
15

Mhubiri kutoka nchini Kenya, Eliud Wekesa maarufu kama ‘Yesu wa Tongaren’, ameendelea kuzuiliwa katika kituo cha Polisi cha Bungoma kwa siku nne zaidi hadi upelelezi utakapokamilika.

Mahakama imetoa uamuzi huo siku ya Ijumaa ikisema kwamba uamuzi huo utaruhusu wapelelezi kutoka Kurugenzi ya Makosa ya Jinai (DCI) kukamilisha uchunguzi kuhusu kanisa la Wekesa la New Jerusalem linalokabiliwa na madai ya mafundisho ya kidini yenye kutiliwa mashaka.

Awali, upande wa mashtaka uliomba mhubiri huyo azuiliwe kwa siku saba ili kutoa nafasi ya uchunguzi kuhusu nyumba yake na tabia yake binafsi, ombi ambalo lilikataliwa na Hakimu Mkuu wa Mahakamaya Bungoma, Tom Olando na badala yake kuagiza uchunguzi ufanyike ndani ya siku nne.

Geita: Wapiga simu Zimamoto kuwasalimia askari

Kwa mujibu wa mahakama, uchunguzi utafanyika katika nyumba ya Wekesa ambayo inatajwa kuwa eneo la uhalifu, kanisa lake na pia kumpima mhubiri huyo afya yake ya akili.

‘Yesu Wa Tongaren’ anakabiliwa na mashtaka yakiwemo ya itikadi kali, utakatishaji fedha, kupata, kumiliki au kutumia mapato ya uhalifu pamoja na kuandika au kutamka maneno kwa nia ya kuumiza hisia za kidini kinyume na kifungu cha 138 cha Kanuni ya Adhabu.

Send this to a friend