Kenyatta adai Ruto anatumia muda mwingi kwenye kampeni badala ya kutumikia wananchi

0
37

Vuta nikuvute uliyopo kati ya Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Ruto umeendelea kushika kasi baada ya Ruto kumjibu kiongozi wake katika mkutano wake wa kisiasa.

Rais Kenyatta alimkosoa Ruto kwa kudai kuwa anapoteza muda mwingi kwenye mikutano ya kisiasa akifanya Kampeni za Urais badala ya kuwahudumia wananchi wake.

Akijibu hoja hiyo, Ruto amesema Rais Kenyatta amehusika katika uundwaji wa vyama vidogo vidogo vya kisiasa eneo la Magharibi ili kuwagawanya wananchi kikabila.

Aidha, ameendelea kumkosoa Kenyatta kwa kujitosa kwenye siasa za urithi wake akimtaka kukaa kando na kuwaacha wananchi wajiamulie wao wenyewe.

Hata hivyo mmoja wa wafuasi wa Rais Kenyatta amemtaka William Ruto kuachia nafasi yake na kuongeza kuwa,  tabia anayowaonyesha ni tabia mbaya  na kama hawezi  kumheshimu Rais,  hawezi  kuwaheshimu  wananchi wa Kenya.

Kinara wa NARC-KENYA, Martha Karua amewakosoa Kenyatta na Rutto kwa kujibizana hadharani kuhusu migogoro yao serikalini na kusema kuwa viongozi hao wawili wanawakosea wananchi heshima kwa kurushiana maneno na kuwataka wasuluhishe mgogoro baina yao faragha au wavunjilie mbali Serikali, iwapo hawawezi kudumisha umoja wa kitaifa.

Utengano kati yao ni taswira ambayo imekuwa ikionekana wazi, wakati Rais Kenyatta akisema hafahamu chanzo chake, Ruto amekuwa akimnyooshea kidole cha lawama kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa kuvuruga  mahusiano yao na Rais.

Send this to a friend