Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imefuta shauri la madai lililofunguliwa na mfanyabiashara Patrick Kamwelwe dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na mwenzake William Malecela ‘Lemutuz’.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate baada ya kukubali ombi la mawakili wa Makonda la kufutwa kwa shauri hilo kutokana na mdai kutoonekana mahakamani.
Akiwasilisha ombi hilo, Wakili wa Makonda, Gift Joshua amesema mdai hajaonekana mahakamani kwa mara ya nne mfululizo pamoja na wakili wake, hivyo kuiomba mahakama kuondoa shauri hilo.
Serikali yatangaza jina jipya la Hospitali ya Mirembe
Kamwelwe alifungua kesi dhidi ya Makonda akidai kuporwa gari aina ya Range Rover ambalo alimkabidhi Lemutuz ampatie Makonda ili alitumie wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa wiki mbili kisha amrudishie.
Mfanyabiashara huyo amedai imekuwa tofauti na makubaliano hayo kwani Makonda aliendelea kulitumia gari hilo, hivyo kupitia hati ya madai aliomba kulipwa TZS milioni 240 za usumbufu pamoja na gharama ya kulitumia gari hilo kinyume na makubaliano.