Kesi ya Mange Kimambi yaahiridhwa hadi Januari, 2026

0
61

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwanaharakati wa Tanzania anayeishi Marekani, Mange Kimambi hadi Januri 28 2026.

Wakili wa upande wa Jamuhuri, Clemence Kato ameileza mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika hivyo ukaomba shauri kupangiwa tarehe nyingine.

Mange Kimambi anakabiliwa anashitakiwa kwa tuhuma za utakatishaji wa fedha kiasi cha TZS milioni Sh138.5 ambapo inadaiwa kati ya Machi 1 na Machi 31, 2022, katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, Mange alijipatia fedha hizo akifahamu kuwa fedha hizo ni zao la uhalifu.

Aidha, inadaiwa pia alizipata fedha hizo kwa kufanya kazi ya uandishi wa habari bila kibali pamoja na kuzidai kwa vitisho.

Send this to a friend