Kesi ya Mdee na wenzake yahairishwa hadi Machi 2023

0
41

Kesi iliyofunguliwa na wabunge 19 wakipinga uamuzi wa CHADEMA kuwafukuza uanachama, imeahirishwa na Mahakama Kuu baada ya wakili anayewakilisha CHADEMA, Peter Kibatala kuhudhuria vikao vya Mahakama Kuu vya usikilizwaji wa kesi za jinai vinavyofanyika mkoani Mwanza.

Akizungumza wakili anayemwakilisha Halima Mdee na wenzake 18, Edson Kilatu leo Desemba 6 amesema shauri hilo lilikuja kwa ajili ya usikilizwaji na mahakama hiyo imepanga kusikiliza shauri hilo Machi 6 na 9, 2023.

“Wakili Kibatala aliomba udhuru na kutujulisha pamoja na mahakama yenyewe kutokana na sababu hiyo ya msingi mahakama hili imeridhia ihairishe shauri hili,” amesema Kilatu.

Kilatu amesema kwa sasa mahakama inaenda likizo na baada ya likizo hiyo itaanza vikao vya Mahakama Kuu kwa ajili ya usikilizwaji wa kesi za jinai.

Send this to a friend