Kiama kwa Askari wanaoingiza mifugo hifadhini ili wawataifishe

0
43

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii kufanya ufuatiliaji wa malalamiko ya wananchi kuhusu tabia ya baadhi ya wahifadhi kuswaga mifugo na kuingiza hifadhini kwa lengo la kuitaifisha na kujipatia fedha.

Ameyasema hayo Aprili 27, 2023 bungeni jijini Dodoma wakati akitoa ufafanuzi kuhusu changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika kusimamia masuala ya uhifadhi na namna ambavyo Serikali imekuwa ikizishughulikia changamoto hizo.

Wanafunzi asilimia 97 wafeli mtihani Shule Kuu ya Sheria

Aidha, Majaliwa ameielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii ichukue hatua kali kwa watumishi wa hifadhi watakaobainika kukiuka sheria na taratibu, kwa kufanya vitendo visivyokubalika ikiwemo kuwadhulumu wafugaji wanaoishi kwenye maeneo hayo.

Mbali na hayo, ameagiza operesheni zote zifanyike baada ya wananchi waishio maeneo ya hifadhi kushirikishwa na kupewa taarifa za kutosha kabla ya kufanyika na sio kwa kuwavizia.

Send this to a friend