KIBO GOLD Yarudi tena Kanda ya Kaskazini

0
21

Wakazi wa kanda ya mikoa ya kaskazini ya Arusha, Tanga, Manyara na Kilimanjaro wamekoshwa baada ya bia ya KIBO GOLD kurudi tena baada ya kukosekana kwa kipindi cha miaka 5 sokoni.

Kurudi tena kwa bia hii inalenga kudumisha historia ya kipekee kwa SBL kutengeneza bia yenye kilele cha ladha ileile bora na adimu ambapo pia chapa hii imeshuhudiwa kunyakua tuzo mbalimbali za dhahabu kama ya Monde Section kwenye mashindano yaliyofanyika mjini Bordeaux, nchini Ufaransa mwaka 2014.

Mkurugenzi wa Masoko na Uvumbuzi SBL, Anitha Rwehumbiza (wa pili kulia) akitangaza rasmi kwa ishara kurejea kileleni kwa bia ya KIBO GOLD kanda ya kaskazini (Kilimanjaro, Tanga, Arusha, na Manyara) baada ya kutokuwepo sokoni takribani miaka 5 katika hafla iliyofanyika mkoani Kilimanjaro tarehe 24 Julai. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa SBL, Chris Gitau, akifuatiwa na Meneja Uvumbuzi SBL, Bertha Vedastus na wa kwanza kulia ni Meneja Mauzo kanda ya kaskazini SBL, Patrick Kisaka

Bia ya KIBO GOLD sasa inarejea ikiwa na mwonekano maridadi kwa kutengenezwa kwa ubora usio na kifani – ikiwa na viungo vya asilia na kutokuwa na sukari ya ziada na kwa bei ya 1,500/- tu.

Akizungumza katika uzinduzi wa bia hio mwanzoni mwa wiki hii mjini Moshi, Meneja Uvumbuzi wa SBL, Bertha Vedastus, alisema, ‘’Kama SBL tunalenga kupanua wigo wetu wa bidhaa kuhakikisha tunakidhi mahitaji ya wateja wetu popote walipo. Na kama tunavyojua Watanzania tunathamini sana urithi na utamaduni katika kila jambo tunalolifanya. Hivyobasi, tunapotafuta maendeleo katika maisha yetu ya kila siku, ni muhimu kuhifadhi na kuthamini urithi na utamaduni wetu. Na kwayo, uwepo wetu wa muda mrefu katika kanda ya Kaskazini umetufanya kuja na maamuzi ya kina ya kudumisha urithi na ufahari wa kanda hii kupitia bia ya KIBO GOLD.

Meneja Uvumbuzi SBL, Bertha Vedastus (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) akitangaza kurejea kwa bia ya KIBO GOLD baada ya kutokuwepo sokoni kwa miaka 5 kanda ya kaskazini, mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Uvumbuzi SBL, Anitha Rwehumbiza na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara SBL, Chris Gitau. Tukio hilo lilifanyika mkoani Kilimanjaro tarehe 24 Julai.

Bertha aliendelea kuelezea kuwa bia ya KIBO GOLD ina utajiri wa kihistoria na urithi wa ubora ambao kila mtanzania inabidi ajivunie kuuendeleza. Alinukuliwa, ‘ni bia yetu, ya watu wetu na urithi wetu. Tunaamini KIBO GOLD – Kilele Cha Ubora, itaendelea kuwa chaguo la kwanza kwa wapenda bia katika kanda hii nzima’’.

SBL baada ya kutambua mara moja uwezo na thamani ya chapa hiyo ya KIBO GOLD imedhamiria kuirejesha katika mioyo ya wapendwa wa bia kote Ukanda wa Kaskazini. Bia hii yenye sura mpya ya kisasa kwa bia itaongeza mvuto wake kwa soko la ndani na la nje.

Send this to a friend