Kichwa kipya cha treni ya umeme chawasili nchini

0
16

Shirika la Reli Tanzania (TRC) imesema kichwa kipya cha treni ya umeme chenye namba ya usajili E6800-1 kilichoundwa na kampuni ya Hyundai Rotem Company (HRC) kimewasili nchini kutokea nchini Korea Kusini ambapo kina uwezo wa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa pamoja na kuvuta na kulisha umeme kwenye mabehewa yasiyozidi 14 ya abiria kwa wakati mmoja.

Aidha, TRC imesema inatarajia kufanya majaribio ya kichwa cha treni kitakachotumika katika reli ya kiwango cha Kimataifa kati ya Dar es Salaam na Morogoro, na baadaye Dar es Salaam hadi Dodoma baada ya kukamilisha ukaguzi wa kichwa na mafunzo ya uendeshaji kwa madereva mwezi Desemba.

“Mwezi Desemba 2023 TRC inatarajia kupokea vichwa vingine vitatu mpango wa uletaji vitendea kazi utakuwa ukitekelezwa kwa awamu pindi uundwaji wa vitendea kazi unapokamilika. TRC imeshapokea mabehewa 35 kwa ajili ya uendeshaji wa huduma katika reli ya kiwango cha kimataifa,” imesema TRC.

Serikali yabainisha vyanzo vitakavyogharamia bima ya afya kwa wasio na uwezo

Imebainisha kuwa kufikia Septemba mwaka huu mradi wa SGR Dar es Salaam- Morogoro umefikia asilimia 98.6, Morogoro- Makutupora umefikia asilimia 95.41, Makutupora- Tabora asilimia 12.32, Tabora- Isaka asilimia 5.02 na Mwanza- Isaka umefikia asilimia 41.95.

Send this to a friend