Kigoma: Miili miwili ya watoto waliozama mtoni imepatikana

0
37

Miili ya watoto wawili kati ya wanne waliozama kwenye mto Luiche Manispaa ya Kigoma Ujiji, mkoani Kigoma Februari 24, 2023 baada ya mtumbwi waliokuwa wamepanda kupinduka imepatikana.

Akithibitisha kupatikana kwa miili hiyo, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na ukoaji mkoani Kigoma, Jacob Chacha amesema miili ya watoto waliopatikana ni ya Zabibu Jumanne (8) na Ramadhani matatizo (12).

TANAPA yakanusha kujenga lami Hifadhi ya Serengeti

Aidha, Kamanda Chacha amesema vikosi vya jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani humo vinaendelea kuwatafuta watoto wengine wawili ambao hawajapatikana mpaka sasa baada ya mtumbwi huo kuzama.

Wanafunzi hao wanne kati ya sita wa shule ya msingi Kagera wanaoakadiriwa kuwa na umri wa miaka 7-14 walizama na mtumbwi katika mto huo asubuhi ya Februari 24, 2023 wakati wakivuka ng’ambo kuelekea shuleni.

Send this to a friend