Kigoma: Wanafunzi wanne waliozama mtoni wakienda shule asubuhi hawajapatikana

0
35

Wanafunzi wanne kati ya sita wa Shule ya Msingi Kagera wanaoakadiriwa kuwa na umri wa miaka 7-14 mkoani Kigoma waliozama na mtumbwi katika Mto Ruiche asubuhi ya leo Februari 24, 2023 wakati wakivuka ng’ambo kwenda shuleni bado hawajapatikana.

Akizungumza na Swahili Times, Kamishna Msaidizi wa Polisi mkoani humo, ACP Philemon Makungu amesema wakati wanafunzi hao wakivuka maji kuelekea shuleni mida ya saa mbili asubuhi, mtumbwi uliokuwa umewabeba ulizidiwa na maji kisha kugonga bomba la maji linalokatiza mtoni na kutumbukia majini.

Kamanda amesema watoto wawili na aliyekuwa nahodha wa mtumbwi huo, Ndemeye Andrea waliweza kuokolewa na kupatiwa huduma ya matibabu kisha kuruhusiwa lakini mtumbwi huo bado haukuoneka.

Mtaalam: Ukiathiriwa na sumu usinywe maziwa, njoo hospitali au tupigie simu

“Tunaendelea na msako wa kuwasaka kwenye maji ili kuweza kuiokoa hiyo miili lakini bado haijaibuka. Tunaendelea mpaka tutakapoipata,” ameeleza

Aidha, Makungu ameeleza kuwa tukio la kuzama maji katika mto huo halijawahi kutokea kwa wakazi wa eneo hilo takribani kwa zaidi ya miaka ishirini.

Send this to a friend