Kijana afa maji akishindania TZS 4,000 kwa kuogelea

0
48

Mkazi wa Kitongoji cha Manyala, Kijiji cha Nyabange wilayani Butiama, mkoa wa Mara, Katamala Jackson (29) amefariki dunia kwa kuzama kwenye bwawa baada ya kushindana na wenzake (kubeti) kuogelea ambapo msindi angepatiwa TZS 4,000.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mrakibu Msaidizi Augustino Magere amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa marehemu alikuwa akicheza mpira na wenzake na ndipo walianza kushindana kwenye bwawa.

“Kwa bahati mbaya Katamala alipofika kwenye kina kirefu cha maji alikosa pumzi na kupelekea kufariki dunia. Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi tulifanikiwa kuuopoa mwili huo ambao ulikuwa umenasa kwenye tope katika bwawa hilo,” amesema Kamanda Magere.

Hata hivyo, Kamanda Magere amewapiga marufuku wakazi wa kitongoji hicho kuogelea katika bwawa hilo, na kuwataka viongozi wa Serikali ya kijiji kusimamia maagizo ya Serikali ili bwawa hilo litumike katika matumizi yaliyokusudiwa.

Send this to a friend