Kijana afariki alipokuwa akiwakimbia askari 

0
70

Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Mkacha Mohamed (35) mkazi wa Soya wilaya ya Chemba mkoani Dodoma amefariki dunia baada ya kuanguka na pikipiki akiwa na wenzake walipokuwa wakiwakimbia polisi.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi vijana hao walikuwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi bunda 250 sawa na kilo 119.

Kamanda wa  Polisi mkoa wa Manyara, ACP George Katabazi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo wakati polisi wakiwa katika doria siku ya Jumapili katika kijiji cha Namelock Kata ya Namelock wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.

“Pikipiki hiyo ilipasuka tairi ya mbele wakati wakifukuzana na askari Polisi wa Kibaya ambao waliokuwa kwenye doria baada ya kuhisi kuwa watu hao walikuwa wamebeba magendo na waliposimamishwa na Askari hao hawakusimama ndipo wakaanza kufukuzana kisha pikipiki yao ikapasuka tairi na kuanguka  na kusababisha kifo hicho,” amesema.

Aidha, amesema dawa hizo zilikuwa zinasafirishwa kwenda Wilaya ya Chemba mkoa wa Dodoma kwa usafiri wa pikipiki ambayo haikuwa na namba za usajili.

Send this to a friend