Kijana aiba nguo za ndani za wanawake ili kumzawadia mpenzi wake

0
47

Mwanaume mwenye umri wa miaka 19 anayejulikana kama Joel Kimurgor anayeshukiwa kuiba nguo za ndani za wanawake katika Kijiji cha Tegeyat, Kaunti ya Nandi nchini Kenya amenaswa.

Kwa wiki kadhaa kumekuwa na visa vya wanawake kuripoti upotevu wa nguo za ndani kutoka kwenye kamba nyakati za usiku, ambapo walianzisha zoezi la upekuzi kutoka nyumba moja hadi nyingine ndani ya kijijj hicho.

Kulingana na mzee wa kijiji cha Tegeyat, Kiptanui  Ronoh mtuhumiwa amenaswa Jumatatu akiwa na nguo 20 za ndani za wanawake na aina nyingine ya nguo zikiwa zimefungwa kwenye mifuko nyumbani kwake.

Kenya yakodi ardhi ya kulima mahindi nchini Zambia

Mshukiwa amekiri kuiba nguo hizo kutoka katika nyumba tofauti kijijini hapo ili kumfurahisha mpenzi wake ambaye alimwomba amnunulie nguo mpya za ndani kama njia ya kuonesha mapenzi.

Wakazi wa kijiji hicho wamelaani tukio hilo wakisema kuwa ni chukizo katika jamii ya Wakalenjin kuiba nguo za ndani akidai kuwa michezo hiyo hufanywa na waganga na washirikina.

Send this to a friend