Kijana akamatwa kwa tuhuma za kuiba mtoto tangu mwaka 2020

0
53

Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la  Baraka Masunzu mkazi wa Kibondo mkoani Kigoma amekamatwa mkoani humo kwa  tuhuma za kuiba mtoto tangu mwaka 2020.

Mara baada ya kukamatwa na mtoto huyo katika eneo la Shilabela wilayani Geita mtuhumiwa amesema mtoto huyo alimuokota mkoani Tabora baada ya kutelekezwa na mama mmoja ambaye hakumtambua kwa jina.

Melki Laurenti ambaye ni babu wa mtoto huyo amesema mjukuu wake alipotea tangu mwaka 2020 baada ya mtuhumiwa Masunzu kuondoka naye nyumbani kwake kisha kutokomea kusikojulikana.

“Alikuja nyumbani kutafuta kazi ya kulima na mimi nikampa, alinambia ‘ninaomba hela nikanunue nguo’, nikachukua kama shilingi 20,000, nikamkabidhi akawa ameenda kununua nguo. Aliondoka na mtoto wa miaka miwili na miezi tisa, akawa ameaga anaenda kununua nguo Geita akiwa na huyo mtoto ambaye alimuiba nyumbani kwangu, basi alitoweka mpaka tulienda Polisi tukapewa RB, tukamtafuta mwisho wake ikawa tu tumekaa hivyo hivyo hatukupata jibu lolote,” amesema babu.

Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Moringe katika Halmashauri ya Mji Geita, Meshacky Ngunilla amesema wamemkamata mtuhumiwa huyo baada ya kumkuta na mtoto mdogo baada ya kumhoji na kushindwa kutoa majibu ya uhakika juu ya Mtoto huyo ndipo walipoamua kumkamata na kupeleka katika ofisi za mtaa wa Moringe.

Amesema baada ya kuanza kutafuta wazazi wa mtoto huyo walifanikiwa kuwapata na mara baada ya kufika katika ofisi hizo wazazi wa mtoto huyo walimtambua na kusema mtoto huyo alipotea tangu mwaka 2020.

Send this to a friend