Kijana anayedaiwa kuua madereva bodaboda Akamatwa

0
78

Jeshi la Polisi kupitia Kamanda Kanda maalumu ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema polisi wanamshikilia Iddy Omary maarufu kama ‘Chuma Steel’ kwa kosa la mauaji ya bodaboda wawili.

Akizungumza jijini Dar es salaam Muliro amesema mtuhumiwa huyo amekiri kuhusika na mauaji ya watu wawili ambao ni bodaboda ambapo mmoja alikodiwa Aprili 16 eneo la Dege Kigamboni na kupigwa na kitu Kizito kichwani kilichopelekea kifo chake kisha kupora pikipiki yake aina ya boxer yenye namba MC186XX.

Aidha Kamanda Muliro ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo amekiri kuhusika na mauaji ya kijana mwingine aliyefahamika kwa jina la Mkapa Nuru anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 21 hadi 25 eneo la Kigamboni Visikini Agosti 27, 2021.

Hata hivyo Mtuhumiwa Pamoja na wenzake walikiri na kuonyesha pikipiki ya marehemu huyo ilipo, na baada ya Polisi kufika eneo wanalofanyia mauaji walikuta baadhi ya viungo na fuvu la kichwa cha binadamu.

Chanzo: Gazeti la Uhuru

Send this to a friend