
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia kijana aitwaye Piere Saimon (20), mkazi wa Nzuguni B kwa tuhuma za kubaka wanawake wanne wa mtaa huo October 5, 2025.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alikuwa akiingia kwa siri katika nyumba anayoishi mwanamke anayemlenga, na kutekeleza kitendo hicho kwa kutumia vitisho vya kujeruhi.
“Katika uchunguzi wa awali uliofanywa na Jeshi la Polisi, imebainika kuwa Mtuhumiwa huyo anaishi katika nyumba moja na watu wengine 13, kwa sasa zinafanywa taratibu za kisheria ambazo zikishakamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani,” imeeleza taarifa ya polisi.
Aidha, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu pamoja na kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi ili kudumisha amani na usalama katika jamii.
Vyombo vya dola kwa kutoa taarifa za uhalifu na Wahalifu pamoja na kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi ili kudumisha amani na usalama katika jamii” – Polisi Dodoma.








