Kijana wa miaka 19 ajitosa Urais Uganda
Miezi kadhaa kuelekea uchaguzi mkuu wa Uganda utakaofanyika mwaka 2021, kijana mwenye umri wa miaka 19 amejitokeza na kuchukua fomu ya kugombea ofisi hiyo ya juu nchini humo.
Hillary Kaweesa amesema kuwa amewahi kuwa kiongozi na hivyo anakidhi vigeo vyabkuongoza nchi.
Kukidhi vigezo atalazimika kuwa na milioni 20 za Uganda kama ada ya uteuzi.
Pia atatakiwa kukusanya saini 100 za wadhamini katika kila wilaya ambapo taifa hilo lina zaidi ya wilaya 100.
Katiba ya nchi hiyo inaruhusu rai mwenye umri zaidi ya miaka 18 kugombea Urais.
Wengine watakaochuana kwenye nafasi hiyo ni Mbunge, Bobi Wine, Henry Tumukunde na Rais Yoweri Museveni ambaye atatetea nafasi yake.