Kijana wa miaka 30 aeleza alivyogharamia safari ya kutembelea nchi zote duniani

0
42

Imeamchukua Drew Binsky safari za  ndege 1,458 na safari za basi na  treni 1,117 kutimiza ndoto yake ya kufika katika nchi zote duniani, mzunguko alioufanya ndani ya miaka 10.

Akiwa katika nchi ya mwisho, Saudi Arabia amesema kuwa amefanikiwa kuzunguka katika nchi 197 (nne kati ya hizo hazitambuliwi na Umoja wa Mataifa ambazo ni Palestine, Taiwan, Kosovo na Vatcan).

Katika safari hiyo amesema kwa wastani alikaa kwenye kila nchi kwa wiki moja, lakini kwa kiangalia nchi moja moja, kuna nyingine alikaa miezi mitatu, nyingine alikaa miezi sita kama vile Vietnam, Ufilipino, Thailand, Korea Kusini na Jamhuri ya Czech.

Kufanikisha safari zake katika baadhi ya nchi alizokwenda alifanya kazi kwa mfano alifundisha lugha ya Kiingereza nchini Korea ambapo alikuwa akilipwa TZS milioni 4.3 kwa mwezi.

Mwaka 2015 alijiunga Snapchat na kupata udhamini wa makampuni kadhaa ambayo yalimlipa zaidi ya TZS milioni 10 kwa ajili ya kufanya stori za Snapchat katika mashindano ya Olympic ya Rio nchini Brazil. Kwa mwaka huo chanzo chake kikubwa cha mapato kilikuwa Snapchat ambapo aliweza kuingiza zaidi ya TZS milioni 60.

Pia kupitia blogu yake kushirikiana na hoteli na mashirika ya ndege ili kurahisisha safari zake. Kwenye safari zake alifanya video ambapo kwa video 300 za kwanza, hazikumuingia fedha yoyote, lakini akiwa Bangkok alifanya video ambayo ilimuwezesha kupata zaidi ya TZS milioni 20 kupitia matangazo.

Kupitia YouTube sasa anaweka video zake ambapo anapata kati ya TZS milioni 4 hadi 8 kwa mwezi.

Pia anauza programu za  maelezo ya safari kwa TZS 300,000, hivyo kumfanya kuwa na vyanzo mbalimbali vya mapato.

Amesisitiza kwamba katika safari zake, hupanda ndege daraja la uchumi, hulala kwenye hoteli za kawaida na kula sehemu za bei nafuu na kwamba, kuongezeka kwa kipato hakumfanyi aishi maisha ya anasa.

Miongoni mwa changamoto alizopitia ni pamoja na usafiri akiwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, sumu ya vyakula akiwa nchini Yemen, Iran na India.

Send this to a friend