Kikundi cha uhalifu ‘vibeberu.com’ chabaka wananchi mchana

0
43

Kikundi cha ubakaji maarufu kama ‘Vibeberu.com’ kilichopo Kijiji cha Ipinda Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, kimezua taharuki baada ya kudaiwa kufanya vitendo vya ubakaji kwa watoto.

Inadaiwa kikundi hicho kimekuwa kikifanya vitendo hivyo vya ubakaji mchana kweupe hali inayowatia hofu wakazi wa eneo hilo.

Akizungumza mmoja wa walimu wa Shule ya Msingi Ipinda (jina limehifadhiwa) amesema kitendo cha walimu kuwaagiza wanafunzi kuwahi saa 12 asubuhi kushika namba shuleni, kimechochea hatari ya watoto kubakwa, hivyo ameomba wanafunzi waongezewe muda walau saa moja asubuhi.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Erick Komba amesema idadi ya watoto walioripotiwa kubakwa ni zaidi ya watoto 8 ambapo Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini watuhumiwa na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria.

Send this to a friend