Kimbunga CHIDO chasababisha maafa Msumbiji

0
29

Kimbunga kilichopewa jina la CHIDO kimetua katika jimbo la Kaskazini mwa Msumbiji na kupelekea mvua na upepo mkali ulioharibu makazi ya watu pamoja na kuharibu mazingira.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia Watoto UNICEF, limesema kiwango kamili cha uharibifu bado hakijulikani, lakini miji na vijiji vitakumbwa na tatizo la ukosefu wa shule na huduma za afya kwa muda usiojulikana.

Kabla ya kuwasili Msumbiji, kimbunga Chido kilisababisha hasara kubwa katika kisiwa cha kilichopo sehemu ya Ufaransa cha Mayotte siku ya Jumamosi, na idadi ya vifo inasemekana huwenda ikafikia zaidi ya mia moja.

Nchini Tanzania, Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ilitoa tahadhari ya uwepo wa kimbunga hicho katika Bahari ya Hindi, Kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar, na kueleza kuwa upo uwezekano mdogo wa matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa itakayoambatana na upepo mkali na mawimbi makubwa ya Bahari kwa maeneo ya Mtwara na maeneo ya jirani hususan kati ya Desemba 14 na 16, 2024.

Send this to a friend