Kimbunga Jobo chapungua kasi ghafla

0
45

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imesema kuwa Kimbunga Jobo kipo umbali wa 200km kutoka Kisiwa cha Mafia  na kwamba kimepungua kasi ghafla na kufikia kasi ya 18km kwa saa baada ya kufika kwenye mazingira yenye upepo kinzani.

TMA imesema kuwa Kimbunga ‘Hafifu’ Jobo kinatarajiwa kusababisha mawimbi makubwa baharini na mvua kubwa katika maeneo machache hususani ya ukanda wa Pwani, kadiri kinavyosogea nchi kavu.

Maeneo yanayotarajiwa kuathirika moja kwa moja ni pamoja na mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam na kisiwa cha Unguja.

Kufuatia uwepo wa kimbunga hicho, mamlaka za Zanzibar zimesitisha safari za bahari na shughuli nyinginezo hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.

Send this to a friend