Kinana akerwa na utitiri wa trafiki barabarani

0
39

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Abdulrahman Kinana amemsihi Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camillus Wambura kufanya tamthmini juu ya hali ya wingi wa trafiki walioko kwenye miji wanaosababisha kero barabarani.

Kinana amesema shughuli hazifanyiki ipasavyo kutokana na askari wa usalama barabarani kuwa kila mahali, hali inayopelekea kusimamishwa kila baada ya hatua kadhaa unapokuwa njiani.

Aliyewazalisha wanawake wawili kwenye geti la zahanati ajengewa nyumba

“Hii ni nchi pekee ambayo trafiki wamejazana humo kila mahali, kilometa 1 trafiki, kituo cha basi trafiki. Namuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi wafanye tathmini watu wapumue wafanye shughuli zao” amesema.

Aidha, amesema wananchi wanatambua umuhimu wa trafiki katika kuhakikisha usalama wao, lakini biashara nyingi zinaharibika na wengine kuchelewa katika shughuli zao kutokana na usumbufu huo.

Send this to a friend